Je, umewahi kujiuliza kwa nini baadhi ya watu wanaonekana kuwa na majibu ya kila tatizo? Kwa nini wengine wanafanikiwa kwa urahisi wakati wengine wanakwama kwenye vikwazo vidogo?
Jibu siyo kwamba wao wamezaliwa na akili nyingi kuliko wengine. Jibu liko kwenye jinsi wanavyofikiri.
Watu tunaowaita "mageneus" kuanzia Leonardo da Vinci hadi Elon Musk hawatumii uchawi. Wanatumia mbinu za kiakili (mental models) na mitindo ya kufikiri ambayo inawawezesha kuona fursa pale wengine wanapoona matatizo, na kupata suluhisho pale wengine wanapoona giza.
Habari njema ni hii: Kufikiri kama genius ni ujuzi unaoweza kujifunza.
Leo, tutaenda mbali zaidi ya maneno ya kuhamasisha. Nitakufundisha njia 4 madhubuti, zilizothibitishwa kisayansi na kihistoria, za kubadilisha mtindo wako wa kufikiri kuanzia sasa hivi.
1. Kubali 'Growth Mindset': Acha Kusema "Siwezi," Anza Kusema "Sijaweza Bado"
Badiliko lolote kubwa linaanza ndani ya nafsi yako. Mtindo wako wa kwanza wa kufikiri unahusu jinsi unavyojichukulia wewe mwenyewe na uwezo wako.
Growth Mindset (Mtazamo wa Kukuza): Hawa wanaamini kuwa akili na uwezo vinaweza kuendelezwa kupitia bidii, mafunzo, na uvumilivu. Kwao, kushindwa ni sehemu ya kujifunza, siyo mwisho wa safari.
Mageneus wote wana Growth Mindset. Hawajali kuonekana wajinga mwanzoni, kwa sababu wanajua kuwa mazoezi yatawafanya wawe bora.
- Tambua Sauti ya 'Fixed Mindset': Wakati wowote unapokutana na changamoto na sauti ya ndani inasema, "Siwezi hili, sina kipaji," itambue.
- Jibu kwa 'Growth Mindset': Badilisha usemi huo. Sema, "Sijui jinsi ya kufanya hili bado, lakini ninaweza kujifunza."
- Sherehekea Jitihada, Si Matokeo Tu: Badala ya kujisifu kwa kuwa "mwenye akili," jisifu kwa "kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa."
Kufikiri kwa Misingi ya Kwanza kunamaanisha kubomoa tatizo lolote gumu hadi kwenye ukweli wake wa msingi kabisa (fundamental truths) ambao hauwezi kubomolewa zaidi, na kisha kujenga suluhisho jipya kuanzia hapo.
Mfano: Watu walisema betri za magari ya umeme ni ghali sana na zitabaki kuwa ghali. Musk alibomoa tatizo: "Betri zimeundwa na nini? Kaboni, nikeli, alumini, polima. Tukizinunua hizi kwenye soko la bidhaa na kuziunganisha sisi wenyewe, gharama itakuwaje?" Matokeo yake yalikuwa betri za bei nafuu sana na mapinduzi ya Tesla.
- Tambua Tatizo na Dhana Zake: "Siwezi kuanzisha biashara kwa sababu sina mtaji mkubwa." (Dhana: Biashara zote zinahitaji mtaji mkubwa).
- Bomoa Hadi Kwenye Misingi: Biashara inahitaji nini hasa? Bidhaa/huduma, na mteja anayelipia.
- Unda Ufumbuzi Mpya: Je, ninaweza kutoa huduma (kama ushauri au ustadi) kwa mteja mmoja bila gharama kubwa, na kutumia faida hiyo kukua?
Albert Einstein hakugundua nadharia ya relatovity kwa darubini; aliigundua kwa kufanya jaribio la fikra. Alijiuliza: "Itakuwaje kama nitaendesha boriti ya mwanga? Nitaona nini?" Swali hili rahisi liliongoza kwenye mapinduzi ya fizikia.
Jaribio la fikra ni njia ya kuchunguza hali ngumu, nadharia, au maamuzi kwa kupanga matukio ya kufikirika akilini ili kuona matokeo yake yanayoweza kutokea, bila hatari ya kweli.
- Tumia 'Second-Order Thinking': Usiulize tu, "Nini kitatokea nikifanya hivi?" Uliza, "Na kisha nini kitatokea?" (And then what?). Fikiria athari za mbali za maamuzi yako, siyo matokeo ya papo hapo tu.
- Jaribu 'Inversion' (Kugeuza): Badala ya kuuliza "Nifanye nini ili nifanikiwe?", uliza "Nifanye nini ili nifeli kabisa?" Kisha, epuka vitu hivyo ulivyovigundua.
Wanajua kuwa wazo bora la biashara linaweza kutoka kwenye biolojia, na suluhisho la uhandisi linaweza kutoka kwenye sanaa. Kadiri unavyokuwa na maarifa mbalimbali, ndivyo unavyokuwa na "nukta" nyingi za kuunganisha ili kuunda mawazo mapya.
Leonardo da Vinci alikuwa mchoraji, mvumbuzi, na mwanatomia. Ujuzi wake wa anatomia ulimfanya awe mchoraji bora, na ujuzi wake wa sanaa ulimfanya awe mvumbuzi mwenye maono.
- Soma Nje ya Fani Yako: Kama wewe ni mhasibu, soma kitabu cha saikolojia. Kama wewe ni mwanasayansi, nenda kwenye jumba la sanaa.
- Tafuta Mifumo (Patterns): Unaposoma vitu tofauti, tafuta kanuni zinazofanana. Je, jinsi mti unavyokua inafanana na jinsi mtandao wa kompyuta unavyosambaa?
- Andika Mawazo Yako: Weka daftari la mawazo (idea journal). Andika kila wazo, hata kama linaonekana la kijinga. Baadaye, unaweza kurudi na kuona jinsi mawazo hayo "yanavyoungana."
Mabadiliko hayatatokea kwa usiku mmoja. Lakini ukianza kutumia hata mbinu moja tu kati ya hizi leo, utaanza kuona dunia kwa jicho tofauti. Utaanza kuona suluhisho pale wengine wanapoona vikwazo.
Dunia inahitaji mageneus wengi zaidi. Na genius huyo anaweza kuwa wewe au mimi tuianze safari yakuwa magenius sasa!.



